0
Tafsiri ya snitch ni mnafiki /.. Yule ambae akihisi umekosea kwa sababu anazozijua yeye hakuchani kwa sababu hana uhakika ila ila anaenda kuongea kwa wana.. Jamaa siku hizi kawa hivi kawa vile. Snitch huwa hupendi kukosolewa anapenda tu kujazwa kichwa na kusapotiwa kwa kila kitu.. Snitch anaweza kua mtu yeyote bila kujali itikadi. rafiki mnafiki /mwanaharakati mnafiki /M"CHIZI " mnafiki na kadhalika. Sifa kubwa zaidi ya Snitch ni kujishitukia maana ana tabia ya kuficha makucha yake kama paka kwa hyo ukiongea tu chochote kinachohusisha tabia zake atahisi umemsema yeye na hapo ndipo huonesha usnitch wake kwa kujielezea kwa wana Ili uonekane wewe ndo mwenye kosa kabla ukweli haujajulikana.. Snitch ni mwizi anayeiba kwa mwanajeshi akiona kimenuka anakimbilia kituo cha polisi.. Snitch bwana hahaha "ana stress saaaana". Kiasi kwamba akiona hii status lazima aseme nimemzungumzia yeye, nimemchana FB wakati mwenyewe nimetoa tu maana ya Snitch sababu masnitch tunaishi nao lakini wengi hawatambui. STOP SNITCHING.

Post a Comment Blogger

Theme images by sebastian-julian. Powered by Blogger.
 
Top