Mwaka 2014 stori kubwa kutoka nchi za
West Africa zilizokaa sana kwenye vichwa vya habari ni ishu ya ugonjwa
wa Ebola.. watu waliofariki ni zaidi ya 5,000, wengine ambao walipata
maambuizi ya ugonjwa huo ni zaidi ya watu 10,000… changamoto kubwa
ilikuwa kupatikana kwa dawa na chanjo ya kuzuia ugonjwa huo.
Ian Crozier alikua ni mmoja wa madaktari
waliojitolea kwenda Sierra Leone kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa
wa Ebola.. muda wake ulipoisha alirudi nyumbani kwao, Atlanta Marekani
ambako waligundua kuwa ana maambukizi ya Ebola, akawekwa kitengo maalum
kwa ajili ya matibabu.
Miezi michache imepita toka Dr. Crozier
atibiwe, stori kwenye headlines leo inamhusu tena yeye.. amegundulika
kuwa na kirusi cha Ebola kwenye jicho la kushoto.
Utafiti unaonesha Dr. Crozier hawezi
kumuambukiza mtu yoyote kirusi hicho, tofauti na ilivyozoeleka kwamba
mtu mwingine akigusana na mgonjwa anapata maambukizi pia.
Uchunguzi bado unaendelea japo inaonekana kama Dr. Crozier asipopatiwa matibabu mapema huenda akapata tatizo la upofu.
Dr. Crozier ni mgonjwa wa kwanza kuugua Ebola mara mbili mfululizo.


