Viongozi wa Kijiji cha Mavanga akiwemo mwenyekiti wa kijiji, Bw.
Hilmar Mpambichaka (Chadema) kulia wakipokea misaada ya vifaa vya
ujenzi toka kwa mbunge Filikunjombe kushoto.
Wananchi wa Mavanga wakiwa wamepanda juu ya magari na miti kumwona mbunge Filikunjombe .
Wananchi wakiwa juu ya miti wakifuatilia hotuba ya mbunge wao Deo Filikunjombe .
Mbunge Filikunjombe akifurahia jambo wakati mkazi wa Mavanga akimtaka kuwa mbunge hadi atakapochoka yeye.
Mwanahabari wa kituo cha Radio Best Ludewa Deo Nyoni akiwa makini kufuatilia matukio
Wananchi
wa Mavanga wakiwa wamebeba kitanda cha kujifungulia wanawake
wajawazito kilichotolewa na mbunge Filikunjombe kitanda chenye thamani
ya Tsh milioni 5.2
Mwenyekiti wa kijiji Cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akimpongeza mbunge Filikunjombe kwa misaada yake Paroko wa kanisa la Anglicana kushoto akipokea msaada wa bati 300 kutoka kwa mbunge Deo Filikunjombe
Mbunge Filikunjombe kati akikabidhi saruji kwa ajili ya shule ya msingi kijiji cha Mavanga Saruji iliyotolewa na mbunge Filikunjombe Mavanga Mbunge Filikunjombe akikabidhi kitanda cha wanawake wajawazito kujifungulia Mbunge Filikunjombe akiwakabidhi wajawazito kitanda cha kujifungulia Mwenyekiti wa kijiji cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akiwa amepokea msaada wa Darubini toka kwa mbunge Deo Filikunjombe Filikunjombe akiwahutubia wananchi wa Mavanga Wananchi Mavanga wakiwa katika foleni ya kuuliza maswali na kumpongeza mbunge wao
Mbunge Filikunjombe akimkabidhi mpira kijana wa Chadema kijiji cha Mavanga Kijana wa Chadema akimpongeza mbunge Filikunjombe Wananchi Mavanga wakimkabidhi zawadi ya kuku mbunge wao Filikunjombe Mbunge Filikunjombe akipokea zawadi ya mbuzi toka kwa vingozi wa kanisa la Anglicana baada ya kuwasaidia bati 300 za ujenzi wa kanisa Mwenyekiti wa kijiji cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akimongeza mbunge Filikunjombe Filikunjombe akizungumza na mlemavu aliyefika katika mkutano wake
Wananchi wa kijiji cha Mavanga wakiwa wamembeba mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe
Msafara wa mbunge Filikunjombe kijiji cha Mavanga Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akiwapungia mikono wananchi wa kata ya Mavanga
Waendesha boda boda wakiongoza msafara wa mbunge Filikunjombe kwa mbwembwe Mbunge Filikunjombe akiwasikiliza wanafunzi katika kijiji cha Mavanga Mbunge Filikunjombe akicheza mpira na wanafunzi hao baada ya kuwapa msaada wa mpira na sukari kwa mwaka mzima
Wasanii wa ngoma katika kijiji cha Mavanga wakishiriki kupiga ngoma na mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kushoto Katibu mwenezi mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya akishiriki kucheza ngoma

Mbunge Filikunnjombe na katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Bw Mgaya wakicheza ngoma
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE
wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe asema baadhi ya
wabunge ,mawaziri na watendaji wabovu serikalini wanakichafua chama cha
mapinduzi ( CCM )
Filikunjombe
alisema kuwa Ccm ni chama makini na kinachopendwa sana ila shida ipo
kwa baadhi ya watu waliopo ndani ya Ccm na serikali ni bomu
mbunge
huyo alitoa kauli hiyo leo katika kijiji cha Mavanga wakati akijibu
maswali ya wananchi na viongozi wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi (
Ukawa) kuhusiana na Ccm kuwateulia wananchi viongozi wasio na sifa
kugombea nafasi mbali mbali.
Alisema
kama kila mmoja angetimiza wajibu wake katika nafasi yake hakuna
mpinzani ambae angechaguliwa ila kuchaguliwa kwa wapinzani ni kushindwa
kwa wale waliowaamini kutoka Ccm kushindwa kuwajibika kwa wananchi
waliowaamini
Filikunjombe
alisema atakuwa mbunge wa mwisho kunyoshewa kidole na watanzania
wakiwemo wananchi wake wa Ludewa kwa kushindwa kuwatumikia wananchi na
chama chake cha Ccm .
Kwani
alisema hakuomba ubunge kwa ajili ya kujinufaisha binafsi ila aliamua
kugombea ili kuwatumikia wana Ludewa kwa kuwapelekea maendeleo hivyo
Kazi Yake kwa sasa hadi mwisho wa ubunge wake ni kuleta maendeleo kwa
wananchi wake na kuona ahadi zake zinatimia kwa muda uliopangwa na si
kujinufaisha kwa wakati.
"
Naomba kwanza mtambue kuwa wabunge wote tulipo fika bungeni kwa mara ya
kwanza tulikopeshwa Tsh milioni 90 kwa ajili ya kununua gari la
kutembelea na Mimi kwa kuwa nilikuwa na gari pesa hizo niliamua kununua
gari la wagonjwa Mlangali ambao hawakuwa na gari la wagonjwa ....lengo
langu kutumikia wananchi na kuwatatulia kero zao si vinginevyo"
Akielezea
msaada huo wa vitu mbali mbali vyenye thamani ya Tsh milioni 40
alivyotoa alisema ni pamoja na kitanda cha kujifungulia wajawazito
chenye thamani ya Tsh milioni 5.2,Darubini ,pesa ya taslimu Tsh milioni 1
bati zaidi ya 500 ,rangi debe 20 ,saruji zaidi 525 na vifaa vingine
vingi kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa miradi mbali mbali ya kijiji na
ujenzi wa makanisa,shule na wodi la wazazi
Awali
viongozi ukawa wa kijiji cha Mavanga kata kata ya Mavanga walimpingeza
mbunge Filikunjombe kwa kuwa mbunge wa mfano Ludewa japo wapo viongozi
wengi ndani ya chama chake ni wabovu.
Mwenyekiti
wa Ukawa Mavanga John Mligo akishukuru kwa msaada huo wa vifaa na fedha
toka kwa mbunge Filikunjombe alisema kama wabunge na viongozi wote
wangefanya kama Filikunjombe kamwe wananchi wasingechukia chama hicho.
Akizungumza
katika mkutano huo mwenyekiti huyo wa Ukawa na mwenyekiti wa serikali
ya Kijiji cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema ) walisema wao
kama viongozi wa upinzani hawana shaka na uwakilishi wa mbunge
Filikunjombe ndani ya jimbo hilo na nje ya jimbo hilo
"
Tumekuwa na wabunge 7 ambao wametangulia kabla ya Filikunjombe ila
uwakilishi wake umekuwa wa kuigwa na wabunge wengine na kama wabunge
kote nchini wangekuwa watendaji hivyo huenda upinzani nchini
usingekuwepo"alisema Mligo
Kwani
alisema kuwa Chanzo cha kijiji hicho kuchagua mwenyekiti wa Serikali ya
kijiji kutoka Chadema ni baada ya viongozi wa ccm kuonyesha kuwa mbali
na wananchi na baadhi Yao kutafuna pesa za michango ya wananchi .
Bw
Mligo alisema shida ndani ya Ccm ni vita ya wenyewe kwa wenyewe ndio
ambayo imekuwa ikiwachanganya wananchi na kujikuta wananchi wanaingia
katika mgawanyiko na kuchagua wapinzani
Alisema
wakati wa kampeni hata wasio na sifa wanataka kuchaguliwa kwa kutumia
rushwa ,hivyo kutaka kwa Ludewa kutambua wazi mbunge anayekubalika ni
Filikunjombe pekee na kuwa hawahitaji mtu zaidi ya mbunge wao
aliyewavusha katika maendeleo
Huku
mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bw Mpambichaka akiwataka
wananchi wa Ludewa kuacha kuonja sumu kwa kubadili wabunge na kuwa
utendaji wa Filikunjombe hakuna wa kumfananisha nae
Alisema
kuwa wamepata kushuhudia utendaji wake ndani ya bunge kupitia kamati ya
PAC kwa kupambana na ufisadi kupitia Escrow na kuwafanya mawaziri zaidi
ya watatu kujiuzulu
Pia
kupitia utendaji wake ndani ya jimbo amefanikiwa kuwavuta wana Ludewa
ambao siku zote walikuwa wakiona aibu kuweka wazi kuwa ni wakazi wa
Ludewa na badala Yake kudanganya kuwa wao ni wazaliwa wa Mkoa wa Ruvuma
kutokana na awali Ludewa kuwa nyuma kwa maendeleo .
"
Toka Filikunjombe ameingia madarakani mwaka 2010 na kuwepo kwa kasi ya
maendeleo ndio tunashuhudia wana Ludewa wakirejea Nyumbani na
kujitangaza kuwa wao ni wakazi wa Ludewa tofauti na zamani wengi
walikuwa wakijificha kwa aibu "
Hata
hivyo alisema wapo wabunge ambao wamekaa majimboni muda mwingi kama
akina Mzindakaya huko Sumbawanga ila siku zote ni mtu wa kueleza jinsi
alivyofanya Kazi na Mwl Julius Nyerere ila si kujipambanua namna gani
alivyoleta maendeleo jimboni
Kuhusu
misaada mbali mbali iliyotolewa na mbunge huyo kijijini hapo mwenyekiti
huyo alisema kwa mara ya kwanza toka wabunge 7 waliopita kijiji hicho
kimepata kupata misaada mingi kutoka kwa mbunge