Mkenya Aliyeorodheshwa Zaidi ya Aliko Dangote Ana Mipango Na Mombasa..... Ni Mipango Gani?
Aliorodheshwa kua nambari mbili katika orodha ya watu wenye waono makubwa Afrika. Nambari moja alikua Rais wa Tanzania, John Kapombe Magufuli . Katika orodha hio Joe Kariuki aliwapiku vigogo tajika barani kama vile tajiri mkubwa Africa, Aliko Dangote.
Joe amejulikana sana katika tasnia ya burudani alipokua akimiliki Candy n Candy kabla ya kuanza mradi wa AMSHA MAMA ambao ni mradi wa kuhamasisha akina mama na kuwawezesha kufanya biashara na kujiendelesha kimaisha.
- Wikendi iliyoisha, Joe Kariuki alikua hapa mkoani akiwa ni katika hali ya matayarisho ya tamasha kutambulisha mradi huo hapa mkoani. Joe alitembelea vikundi vya kina mama eneo la Frere town akiwa pamoja na mkuu wa radio, Pilipili FM, Chris da Bass, mtangazaji wa PiliPili FM Gates Mgenge pamoja na MCA mtarajiwa wa wadi ya Frere, Charles Kitula na aliweza kuwapa wanawake wawili pesa talim kama mtaji wa kuanza biashara ili wweze kujitegemea.
CRDT MACHAMPALI
Post a Comment Blogger Facebook
Post a Comment