 |
Wagombea waliobaki kwenye
kinyanganyiro cha kuwania urais nchini Marekani, wanang'ang'ania kura
muhimu zaidi za mchujo hii leo katika jimbo la New york. Likiwa moja ya
majimbo makubwa nchini Marekania lina ushawishi mkubwa kwa wagombea
wote.
Kwa wagombea wa chama cha Democtrats Bernie Sanders
amelelewa mjini New York naye Hillary Clinton amekuwa seneta katika
jimbo hilo.
Kwa upande wa Republican mgombea mkuu Donald Trump ni mwenyeji wa jimbo hilo.
Ananuia kupata ushindi dhidi ya mshindani wake mkuu Ted Cruz, Lakini amekosoa mbinu ya kumchagua mgombea wa chama. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Wagombea hao wote wamekuwa kwenye kampeni ya kuwarai wapiga kura.
Clinton aliwaambia wapiga kura kuwa hatachukulia chochote kwa msaha huku
kwa upande wa Republican Trump akisisitiza mapenzi yake kwa jimbo la
New York.
Mshindani wake mkuu Ted Cruz hatarajiwi kufanya vyema baada ya kukosoa sera za Trump mapema kwenye kampeni.
CRDT BBC
Post a Comment Blogger Facebook
Post a Comment