






Mimi na viongozi wenzangu wa UKAWA tumepata fursa ya kutoa heshima zetu kwenye kaburi la Marehemu Mzee Peter Kisumo kijijini kwake Usangi, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Mzee Kisumo alifariki tarehe 3/8/2015 na kuzikwa tarehe 13/8/2015. Nilipanga na kujitahidi kushiriki mazishi ya mzee wetu, lakini kwasababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu, ilishindikana.
Kwa niaba ya wenzangu, ninawashukuru kwa dhati wanafamilia ya Kisumo kwa kutupa heshima hii ya kutoa heshima zetu kwa Mzee huyu ambaye alikuwa muasisi wa TANU na CCM.
Mungu amlaze mahala pema peponi Mzee wetu.

Post a Comment Blogger Facebook
Post a Comment