




Mazishi
ya diwani wa viti maalumu jijini Arusha,marehemu Belina Kabuje ambaye
alifariki hivi karibuni katika hospitali ya rufaa ya KCMC mjini Moshi
jana yalitawaliwa na huzuni na hisia mbalimbali mara baada ya familia ya
marehemu kuzuiwa isipokee fedha za rambirambi.
Fedha
hizo zilizuiwa na meya wa halmashauri ya jiji la Arusha,Gaudence Lyimo
wakati akitoa salamu za rambirambi ndani ya kanisa Katoliki Parokia ya
Roho Mtakatifu Ngarenaro wakati mwili wa marehemu ulipofikishwa kwa
ajili ya ibada.
Akizungumza
wakati akitoa salamu hizo bila kutaja kiasi chake meya huyo alisema
kuwa fedha zote zilizokusanywa kama rambirambi ya marehemu
hazitakabidhiwa mbele ya familia yake hadi pale utaratibu wa kufungua
akiba utakapokamilika.
Alisema
kuwa lengo la kuweka utaratibu huo ni kuepusha matumizi mabaya ya fedha
hizo kutumika hovyo huku akisisitiza ya kwamba marehemu enzi za uhai
wake alikuwa mtu mwenye hofu na mashaka .
“Marehemu
enzi za uhai wake alikuwa na hofu sana kuna mambo mengine yalikuwa ni
siri kwa familia lakini alilazimika kutushirkisha sisi madiwani”alisema
Lyimo
Hatahivyo,katika
hali isiyo ya kawaida baadhi ya waombolezaji waliohudhuria kanisa hapo
walijikuta wakipiga makofi kushangilia hotuba ya meya huyo pale
alipotamka ya kwamba mali za marehemu huyo kamwe hazitaguswa na mtu
yoyote kwa kuwa kuna wosia umeachwa na marehemu.
Naye,mwenyekiti
wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM(UWT) mkoani Arusha,Flora Zelothe
aligusa hisia za watu kanisani hapo mara baada ya kutamka kwamba
marehemu aliacha wajukuu watatu ambao alikuwa akiwahudumia na kudai
kimsingi wanapaswa kutambuliwa na familia.
Hatahivyo,paroko
wa kanisa hilo,Anchi Mpota akiendesha ibada ya kumuombea marehemu huyo
aliwataka watu kuondoa tofauti zao za kidini,kikabila na kisiasa kwa
madai kwamba zitawagawa.
“Kwa
hali ilivyo sasa amani tuliyonayo tusiichezee tuondoe tofauti zetu za
kidini,kisiasa na kikabila kama tukiziendekeza basi zitatugawa”alisema
paroko huyo
Post a Comment Blogger Facebook
Post a Comment