
Verse 1:
Ilikua Manchester bar,Mida ya saa 9,Machizi wanapanga dili kwenda kuliza,Ikaibuka Rav 4 Ndani imejaa Masniper,Bar ikazungukwa,watu wakatekwa kama viper,Lala chini,Mikwasa imezunguka kila kona,Raiaa kule ndani hawakujua wangepona,Akataitiwa mikono__akapigwa bangili,Mchizi ni pro akaanza kudai wakili,Akili ya jela na mtaa mara 2,walikua wanataim wanten ya afgem na dili,Akashikwa shati kaptura mpaka kwenye Pira,Tumboniii vijana mahabusu aliwa....., Akaingizwa kwenye ndinga Kwa mahojiano zaidi,Wakampeleka usa wanakopelekwa magaidi,mahojiano yanafanyika mchizi akiteswa sana,Kapigwa singe ya mbavu lakini bado kabana,Wazee wakaona anapoteza muda wao,Robbery man huyu so wa roba za mbao,Taarifa ikapelekwa kwa ndugu wa tumbonii,Alikutwa kia akiwa na matundu ya risasi tumboni
Chorus:
Tumboniii Alikua Nyapara wa Jela ya Arusha,Tumboniii Nyamera ambae huezi kumrusha,Tumboniii Business Man Jiji zima,Dakika za mwisho wazee walimzima!!
Verse 2:
Ni jirani na Jcb kimandolu alipokaa,Tabia zilifanana na ile ya Nyokaa,Sema Tumboniii maisha yake yote kaishi jela,Kajenga manyumba kibao kipindi yuko jela,Bana duka mc Tumboniii ndo bidhaa,Utapata kila kitu sero so unashangaa,Mamaake akienda mcheki anapewa fungu,aje endeleza kitaa kombe kwa machungu,Kimandolu nyumba kibao za kupanga zake,---------Usiombee uwe adui yake,Mfanyabiashara maarufu ndani ya sero,anao mtandao mkubwa wa makachero,Akikaa mtaa mwezi--utafkiri miaka 9,Jela inamwita lazma aanzishe visa,Tumbonii alikua mshkaji mkubwa na daaii,Rest in peace kamanda amedie,Safariii ni braza ake tumbonii wa damu,Hiyo combination wazee hawana hamu,Kimandolu ndo station kwa kina ambaa,Alikutwa karibu na kia ubongo umesambaa!!!
Repeat Chorus:

Post a Comment Blogger Facebook
Post a Comment