Chama
cha soka cha England FA, kimeipiga faini ya pound 200,000 klabu ya soka
ya Aston Villa, kwa kitendo cha mashabiki kuvamia uwanja kwenye mechi
ya robo fainali ya FA Cup dhidi ya West Bromwich Albion.
Katika
mtanange huo uliopigwa March 7 kwenye dimba la Villa Park, mashabiki wa
Aston Villa waliingia uwanjani wakati wachezaji walipopata majeraha na
hata mwisho wa mchezo huku viti vikirushwa kutoka kwa mashabiki
waliokuwa wamesimama mbali.FA inasema klabu hiyo imeonywa vikali hasa juu ya mwenendo wake katika siku zijazo. Lakini kwa upande wao Villa waliomba msamaha baada ya mechi kuisha na kuongeza kuwa ushindi wao walioupata siku hiyo ulitiwa doa na vitendo vya wale walioshindwa kujizuia wao wenyewe.
Naye boss wa West Brom Tony Pulis amewakosoa walinda usalama wa uwanja huo na kuongeza kuwa usalam wa wachezaji wake ulikuwa mashakani.

Post a Comment Blogger Facebook
Post a Comment