Zaidi ya Bunduki 200 zakamatwa Kiteto
Na. Mohamed Hamad Kiteto
Matukio ya kihalifu yanayoendelea kujitokeza wilayani Kiteto mkoani Manyara yamelazimu Jeshi la Polisi wilayani humo kukusanya silaha aina ya bunduki zinazomilikiwa kihalali na isivyo halali ili kubaini zilizotumika kufanya uhalifu
Zaidi ya bunduki 200 za aina tofauti zikiwemo Raifo,Shotigan,na Magobole zimekusanywa wilayani humo kwa lengo la kufanya uchunguzi kama zimehusika katika mauaji ya watu saba yaliyotokea hivi karibuni katika vijiji vya Chekanao na Matui
Awali akizungumza na vyombo vya habari Deosdedit Nsimeck Kamanda wa Polosi wa Mkoa wa Manyara mjini Kibaya alisema hatua hiyo inasaidia kubaini silaha zinazofanya  matukio ya kihalifu  katika maeneo mbalimbali Wilayani humo
“Silaha hizo toka kwa wananchi tumeamua kuzikusanya zikiwemo zile zinazomilikiwa kihalali na isivyo halali ili kudhibiti vitendo vya kihalifu vinavyoendelea kujitokeza vikiwemo vya mauaji ya mara kwa mara”alisema Nsimeck
Wananchi na viongozi katika maeneo tofauti wamepongeza kitendo hicho wakisema hatua hiyo ni busara iliyotumika ambayo itakomesha mauaji pamoja na kuwepo kwa changamoto kubwa katika kuzipata huko vijijini
“Wakati mwagine mmiliki wa Silaha husika kihalali analazimika kuingia mitini akiwa hana nia ya kuikabidhi lakini baadaye anaagizia mke wake kwenda kuikabidhi kutokana na sababu zao mbalimbali” alisema mmoja wa maafisa hao
Kwa upande wake Emanuel Papian mjumbe wa NEC (CCM) Taifa akizungumzia hatua hiyo alisema matukio hayo yatapungua  kutokana na jitihada hizo na kulitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha watuhumiwa wanafikishwa mahakamani
“Utakuta mhalifu anafanya atakavyo mf. mauaji yanayo endelea kutokea Kiteto hutasikia aliyefanya matukio anawajibishwa, na hili linaenda sambamba na kutowajibika kwa viongozi wa ngazo mbalimbali za maamuzi”alisisitiza MNEC huyo
Katika hatua hiyo mjumbe huyo aliwataka wananchi Wilayani Kiteto kujipima kama wanatosha katika nafasi wanazoshikilia ili kuepusha manunguniko kwa wananchi ambayo yanajitokeza kila mara
Natamani siku moja nisikie na kuona wananchi wa Kiteto wanaishi kwa amani na kujivunia viongozi wao waliowachagua kuwa wanasikilizana katika shuhuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo
Mwisho
Theme images by sebastian-julian. Powered by Blogger.
 
Top