
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia katika Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya
Tabianchi, unaoendelea Jijini Lima nchini Peru. Makamu wa Rais
alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio
mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt.
Bilal alizungumzia namna nchi za Afrika zilivyojizatiti katika maazimio
mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi.
Ujumbe wa Tanzania, katika mkutano huo.....
Katibu Mkuu, Ban Ki-Moon, akizungumza katika mkutano huo........
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wenzake wakati walipohudhuria
katika Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi,
unaoendelea Jijini Lima nchini Peru, ambapo alizungumza kwa niaba ya
nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko
ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi
za Afrik zilivyojizatiti katika maazimio mbalimbali yanayolenga
kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi.
Taswira ya kumbi za mikutano hiyo.....
Makamu wa Rais na ujumbe wake .......
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Mjumbe maalum wa Marekani katika masuala ya Mabadiliko
ya Tabianchi, Todd Stern, baada ya kuhudhuria katika Mkutano wa 20 wa
Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaoendelea Jijini Lima nchini
Peru, ambapo alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu
utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Ujumbe wa China, katika mkutano
wa Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Xie
Zhenhua, wakati walipokutana kwa mazungumzo baada ya kuhudhuria na
kuhutubia katika mkutano huo unaoendelea Jijini Lima nchini Peru, ambapo
alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio
mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi.
Makamu
wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na baadhi ya Mawaziri wakati wakitoka katika chumba cha
mkutano huo.
*********************************************************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMUWAKILISHA RAIS JAKAYA KIKWETE KWENYE MKUTANO WA MAZINGIRA (COP20) JIJINI LIMA, PERU DESEMBA 10, 2014
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
jana Desemba 09, 2014 amemuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye
ni Mwenyekiti Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali Barani Afrika kuhusu
Mabadiliko ya Tabia Nchi, kwenye mkutano wa Kimataifa wa Mazingira
Duniani (Cop20) unaofanyika jijini Lima, Peru.
Pamoja
na shughuli nyingine ambazo zimemuhusisha Mheshimiwa Makamu wa Rais
Dkt. Bilal katika Mkutano huo ikiwa pamoja na kuwa eneo la Mazingira
nchini liko chini ya Ofisi yake, Mheshimiwa Dkt, Bilal alipata fursa ya
kutoa hotuba kwa niaba ya Wakuu wa Nchi za Afrika siku ya Ufunguzi wa
Mkutano huo, huku akisisitiza katika hotuba hiyo umuhimu wa kila nchi
kushiriki katika kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi na tena
akaelezea kuwa, hakuna anayeweza kupona kwa kujificha ama kuachia kazi
hii ifanywe na nchi baadhi na akaongeza kuwa, wanaochangia kwa kasi
kubwa kuathiri mazingira wanatakiwa kutambua
kwamba wanayoyafanya hayatawanufaisha milele hivyo nao washiriki kwa
vitendo katika kukabiliana na janga hili kubwa linaloikumba dunia kwa
sasa.
Awali
akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban Ki-moon alieleza kuwa yapo mabadiliko ya tabia nchi ambayo
kimsingi yametengenezwa na binadamu wenyewe na kama binadamu wakiamua
kukabiliana nayo wanaweza
kabisa kuyatokomeza. Pia alifafanua kuhusu nadharia ya nchi
kushirikiana kwa kuwa mabadiliko haya kwa sasa athari zake hazina mipaka
na kwamba nchi zote lazima ziwe katika sehemu ya utatuzi wa tatizo hili
kubwa linaloikabili dunia.
“Tutumie
mapendekezo ya Lima kufungua njia mpya, tuwe na vipaumbele
vinavyotekelezeka na kuonekana, Tutoke hapa Lima na twende kuandika
historia mpya kwa dunia yetu,” alimalizia Ban Ki-moon.
Kwa
upande wa Rais wa mkutano huo (Cop20) Manuel Pulgar-Vida ambaye pia ni
Waziri wa Mazuingira wa Peru, alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha
washiriki wa mkutano huo nchini Peru kwa niaba ya Rais wa nchi hiyo
Mheshimiwa Olanta Humala na kisha akafafanua kuwa nchi ya Peru imepitia
masaibu kadhaa ya kimazingira na hivyo kupata nafasi ya kuandaa mkutano
huu kwao ni heshima na wajibu katika dunia na kwamba anategemea maazimio
ya Lima yasaidie dunia katika kukab iliana na tatizo hili
linalokuwa la mabadiliko ya tabia nchi.
Kauli
ya Mheshimiwa Manuel Pulgar inasadifu ile aliyoitoa pia Christiana
Fugueres, Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa wa Mkakati wa kukabiliana
na Mabadiliko ya Tabia Nchi ambaye aliuambia mkutano huo kuwa, wakati
umefika kwa nchi zote kukabiliana na matatizo ya mabadiliko ya tabia
nchi kwa pamoja kwa kuwa yanachangia kuongeza umaskini na ili jamii
ipate ahueni, basi ni wajibu kwa kila binadanmu kuchukua nafasi yake
katika kukabiliana na hali hii iliyopo.
Katika
tukio jingine, Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata fursa ya kukutana na
Ujumbe kutoka Marekani uliongozwa na Mjumbe Maalum kutoka Serikali ya
Marekani anayehusika na masuala ya Mabadiliko ya Tabia nchi Todd Stern,
ambaye alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuhusu utayari wa serikali
ya Marekani katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi
na kwamba nchi yake itashirikiana nan chi zinazoendelea ikiwemo
Tanzania katika suala hilo. Vile vile Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata
nafasi ya kukutana na ujumbe kutoka Jamhuri ya Watu wa China ulioongozwa
na Mheshimiwa Xie Zhenhua ambaye alizungumzia kuhusu ushirikiano baina
ya nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea katika suala la mabadiliko
ya tabia nchi na akafafanua kuwa Tanzania na China zina uhusiano wa
kindugu hivyo kama kutakuwa na jambo la kipekee baina ya nchi hizi mbili
basi serikali ya China iko wazi kulipokea.
Mkutano
huo pia umehudhuriwa na Rais wa Bolivia Evo Morales, Rais wa Nauru
Baron Waqa, Waziri Mkuu wa Tuvalu Enele Sopoaga, Rais wa Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa Sam Kutesa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki-Moon. Mkutano huu unafanyika wakati dunia ikiwa imeanza kubadili
fikra na misimamo kuhusu namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia
nchi ambapo nchi ambazo awali zilikuwa na misimamo mikali mfano Marekani
na China sasa zimaeza kubadili fikra kuhusu suala hili na kwa sasa
zinaanza kulipa uzito kutokana na athari yake pia kuzikabili nchi hizo.
Pamoja
na Mheshimiwa Makamu wa Rais msafara wa Tanzia pia unawashirikisha
Mawaziri Bilinith Mahenge (Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira) Waziri Fatma Fereji (Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa
Rais SMZ), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mahadhi Juma Maalim pamoja na wataalam wengine wa masuala ya Mazingira
na Maliasili pamoja na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Lima, Peru Desemba 10, 2014